Nehemiah 8:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha watu wote wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa, Ezra aliwasomea sheria ya Mose akiwa mbele ya Lango la Maji tangu asubuhi hadi adhuhuri. Watu wote wakatega masikio yao kusikiliza kwa makini kitabu cha sheria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko hadi adhuhuri, akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Torati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha torati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha watu wote wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa, Ezra aliwasomea sheria ya Mose akiwa mbele ya Lango la Maji tangu asubuhi hadi adhuhuri. Watu wote wakatega masikio yao kusikiliza kwa makini kitabu cha sheria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko mpaka adhuhuri akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko mpaka adhuhuri, akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Torati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha watu wote wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa, Ezra aliwasomea sheria ya Mose akiwa mbele ya Lango la Maji tangu asubuhi hadi adhuhuri. Watu wote wakatega masikio yao kusikiliza kwa makini kitabu cha sheria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pale penye uwanja ulioko mbele ya lango la Maji akawasomea yaliyomo kitabuni, akaanza asubuhi, akamaliza, jua lilipokuwa kichwani, wakawako waume na wake na watambuzi, nao watu wote pia, wakakisikiliza hicho kitabu cha Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha torati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Ezra akawasomea watu wote wanaume na wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa Sheria ya Musa akiwa mbele ya Mulango wa Maji tangu asubui mpaka saa sita za muchana. Watu wote wakatega masikio yao na kusikiliza kwa uangalifu kitabu cha Sheria.