Nehemiah 8:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu waliposikia sheria, waliguswa mioyoni mwao, ndipo wote walipoanza kulia. Hivyo Nehemia aliyekuwa mtawala na Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliowafundisha watu waliwaambia watu wote, “Siku hii ni siku takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, hivyo msiomboleze wala kulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Nehemia aliyekuwa mtawala, Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Msiomboleze wala msilie.” Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Torati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu waliposikia sheria, waliguswa mioyoni mwao, ndipo wote walipoanza kulia. Hivyo Nehemia aliyekuwa mtawala na Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliowafundisha watu waliwaambia watu wote, “Siku hii ni siku takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, hivyo msiomboleze wala kulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Sheria. Ndipo Nehemia Tirshatha, Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwa BWANA Mungu wenu. Msiomboleze wala msilie.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Nehemia aliyekuwa mtawala, Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu. Msiomboleze wala msilie.” Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Torati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu waliposikia sheria, waliguswa mioyoni mwao, ndipo wote walipoanza kulia. Hivyo Nehemia aliyekuwa mtawala na Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliowafundisha watu waliwaambia watu wote, “Siku hii ni siku takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, hivyo msiomboleze wala kulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Nehemia aliyekuwa mtawala nchi na Ezera aliyekuwa mtambikaji na mwandishi nao Walawi waliowatambulisha watu maana walipowaambia watu: Siku hii ya leo ni siku takatifu ya Bwana Mungu wenu! Msiomboleze, wala msilie machozi! Kwani watu wote walilia machozi walipoyasikia maneno ya Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu waliposikia Sheria, wakaguswa ndani ya mioyo yao, halafu wote wakaanza kulia. Hivyo Nehemia aliyekuwa mutawala na Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliofundisha watu wakawaambia watu wote: “Siku hii ni siku takatifu kwa Yawe, Mungu wenu, hivyo musiomboleze wala kulia.