Nehemiah 9:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao, watumishi wake wote na watu wote wa nchi yake; kwani ulijua kuwa waliwakandamiza babu zetu. Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulituma ishara za miujiza na maajabu dhidi ya Farao, dhidi ya maafisa wake wote na watu wote wa nchi yake, kwa kuwa ulifahamu jinsi Wamisri walivyowafanyia ufidhuli. Ukajifanyia jina linalodumu hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe ukaonyesha ishara nyingi na mambo ya ajabu juu ya Farao, na juu ya watumishi wake wote, na juu ya watu wote wa nchi yake; kwa maana ulijua ya kuwa waliwatenda kwa kutakabari; ukajipatia jina kama vile ilivyo leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao, watumishi wake wote na watu wote wa nchi yake; kwani ulijua kuwa waliwakandamiza babu zetu. Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulituma ishara za miujiza na maajabu dhidi ya Farao, dhidi ya maafisa wake wote na watu wote wa nchi yake, kwa kuwa ulifahamu jinsi Wamisri walivyowafanyia ufidhuli. Ukajifanyia jina linalodumu hadi leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulituma ishara za miujiza na maajabu dhidi ya Farao, dhidi ya maafisa wake wote na watu wote wa nchi yake, kwa kuwa ulifahamu jinsi Wamisri walivyowafanyia ufidhuli. Ukajifanyia jina linalodumu hadi leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe ukaonesha ishara nyingi na mambo ya maajabu juu ya Farao, watumishi wake wote, na watu wote wa nchi yake; kwa maana ulijua ya kuwa waliwatenda kwa kutakabari; ukajipatia jina linalodumu hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao, watumishi wake wote na watu wote wa nchi yake; kwani ulijua kuwa waliwakandamiza babu zetu. Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, ulipotoa vielekezo na vioja kwake Farao na kwa watumishi wake wote na kwa watu wote wa nchi yake, kwani ulijua, ya kuwa waliwakorofisha, ukajipatia Jina, kama lilivyo hata leo hivi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe ukaonyesha ishara nyingi na mambo ya ajabu juu ya Farao, na juu ya watumishi wake wote, na juu ya watu wote wa nchi yake; kwa maana ulijua ya kuwa waliwatenda kwa kutakabari; ukajipatia jina kama vile ilivyo leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulifanya miujiza na maajabu mbele ya Mufalme wa Misri, watumishi wake wote na watu wote wa inchi yake; maana ulijua kwamba waliwagandamiza babu zetu. Ukajipatia utukufu unaokuwa mpaka leo.