Nehemiah 9:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uliigawa bahari katikati mbele yao, nao wakapita katikati ya bahari, mahali pakavu. Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatia kama jiwe zito ndani ya maji mengi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukagawa bahari mbele yao, ili waweze kupita katikati yake penye nchi kavu, lakini uliwatupa Wamisri waliowafuatilia katika vilindi, kama jiwe kwenye maji mengi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, mfano wa jiwe katika maji makuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uliigawa bahari katikati mbele yao, nao wakapita katikati ya bahari, mahali pakavu. Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatia kama jiwe zito ndani ya maji mengi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukagawa bahari mbele yao, ili waweze kupita ndani yake penye nchi kavu, lakini uliwatupa Wamisri waliowafuatilia katika vilindi, kama jiwe kwenye maji mengi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukagawa bahari mbele yao, ili waweze kupita katikati yake penye nchi kavu, lakini uliwatupa Wamisri waliowafuatilia katika vilindi, kama jiwe kwenye maji mengi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, kama jiwe katika maji makuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uliigawa bahari katikati mbele yao, nao wakapita katikati ya bahari, mahali pakavu. Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatia kama jiwe zito ndani ya maji mengi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukaitenganisha bahari mbele yao, wakapita pakavu baharini katikati, nao waliowakimbiza ukawatupa vilindini, kama jiwe linavyotupwa katika maji yenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, mfano wa jiwe katika maji makuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uligawanya bahari katikati mbele yao, nao wakapita katikati ya bahari, pahali pakavu. Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatilia kama jiwe zito ndani ya maji mengi.