Nehemiah 9:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa na njaa, ukawapa chakula kutoka mbinguni. Walipokuwa na kiu ukawapa maji kutoka kwenye mwamba. Ukawaagiza kuichukua nchi uliyokuwa umewaahidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika njaa yao uliwapa mkate kutoka mbinguni, na katika kiu yao uliwatolea maji kwenye mwamba. Uliwaambia waingie na kuimiliki nchi ambayo ulikuwa umeapa kuwapa kwa mkono ulioinuliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukawapa chakula toka mbinguni, kwa ajili ya njaa yao, na kwa ajili yao ukaleta maji kutoka mwambani, kwa sababu ya kiu yao, ukawaamuru kwamba waingie katika nchi na kuimiliki, ambayo umeinua mkono wako kuwapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa na njaa, ukawapa chakula kutoka mbinguni. Walipokuwa na kiu ukawapa maji kutoka kwenye mwamba. Ukawaagiza kuichukua nchi uliyokuwa umewaahidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika njaa yao uliwapa mkate kutoka mbinguni na katika kiu yao uliwatolea maji kutoka kwenye mwamba. Ukawaambia waingie na kuimiliki nchi ambayo ulikuwa umeapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika njaa yao uliwapa mkate kutoka mbinguni, na katika kiu yao uliwatolea maji kutoka kwenye mwamba. Uliwaambia waingie na kuimiliki nchi ambayo ulikuwa umeapa kuwapa kwa mkono ulioinuliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukawapa chakula toka mbinguni, kwa ajili ya njaa yao, na kwa ajili yao ukaleta maji kutoka mwambani, kwa sababu ya kiu yao, ukawaamuru waingie na kuimiliki, nchi ambayo umeinua mkono wako kuwapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa na njaa, ukawapa chakula kutoka mbinguni. Walipokuwa na kiu ukawapa maji kutoka kwenye mwamba. Ukawaagiza kuichukua nchi uliyokuwa umewaahidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukawapa vyakula toka mbinguni vya kuzikomesha njaa zao, ukatoa maji miambani ya kuzikomesha kiu zao, ukawaambia, ya kama wataingia katika nchi hii, waichukue, iwe yao, kwa kuwa uliuinua mkono wako, kwamba utawapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukawapa chakula toka mbinguni, kwa ajili ya njaa yao, na kwa ajili yao ukaleta maji kutoka mwambani, kwa sababu ya kiu yao, ukawaamuru kwamba waingie katika nchi na kuimiliki, ambayo umeinua mkono wako kuwapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokuwa na njaa, ukawapa chakula kutoka mbinguni. Walipokuwa na kiu, ukawapa maji kutoka katika jiwe. Ukawaagiza kurizi inchi uliyokuwa umewaahidi.