Nehemiah 9:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata walipojitengenezea sanamu ya ndama na kusema, ‘Huyu ndiye mungu wetu aliyetutoa kutoka nchi ya Misri,’ wakawa wamefanya kufuru kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hata wakati walijitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu na kusema, ‘Huyu ni mungu wenu, aliyewapandisha kutoka nchi ya Misri,’ au walipokufuru sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, hata walipojifanyia ndama ya kusubu, na kusema, Huyu ndiye Mungu wako aliyekupandisha kutoka Misri, tena walipokuwa wamefanya machukizo makuu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata walipojitengenezea sanamu ya ndama na kusema, ‘Huyu ndiye mungu wetu aliyetutoa kutoka nchi ya Misri,’ wakawa wamefanya kufuru kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hata wakati walipojitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu na kusema, ‘Huyu ni mungu wenu, aliyewapandisha kutoka nchi ya Misri,’ au wakati walipofanya makufuru makubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hata wakati walijitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu na kusema, ‘Huyu ni mungu wenu, aliyewapandisha kutoka nchi ya Misri,’ au walipofanya makufuru makubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, hata walipojifanyia ndama ya kusubu, na kusema, Huyu ndiye Mungu wako aliyekupandisha kutoka Misri, tena walipokuwa wamefanya machukizo makuu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata walipojitengenezea sanamu ya ndama na kusema, ‘Huyu ndiye mungu wetu aliyetutoa kutoka nchi ya Misri,’ wakawa wamefanya kufuru kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata hapo, walipojitengenezea ndama ya dhahabu kwa kuziyeyusha na kusema: Huyu ndiye Mungu wako aliyekutoa Misri, waliposema masimango makuu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, hata walipojifanyia ndama ya kusubu, na kusema, Huyu ndiye Mungu wako aliyekupandisha kutoka Misri, tena walipokuwa wamefanya machukizo makuu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
hata walipojitengenezea sanamu ya mwana-ngombe na kusema: “Huyu ndiye Mungu wetu aliyetutoa kutoka katika inchi ya Misri.” Wakakuchukiza sana