Nehemiah 9:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ukawaruhusu kushinda falme na mataifa, ukawafanyia mengi kila upande. Wakaishinda nchi ya Heshboni alikotawala mfalme Sihoni; na tena wakaishinda nchi ya Bashani alikotawala mfalme Ogu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Uliwapa falme na mataifa, ukiwagawia hata mipaka ya mbali. Wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pamoja na hayo ukawapa falme na taifa za watu, ulizowagawia sawasawa na mafungu yao; hivyo wakaimiliki nchi ya Sihoni, naam, nchi yake mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu, mfalme wa Bashani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ukawaruhusu kushinda falme na mataifa, ukawafanyia mengi kila upande. Wakaishinda nchi ya Heshboni alikotawala mfalme Sihoni; na tena wakaishinda nchi ya Bashani alikotawala mfalme Ogu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ukawapa falme na mataifa, ukiwagawia hata mipaka ya mbali. Wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Uliwapa falme na mataifa, ukiwagawia hata mipaka ya mbali. Wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pamoja na hayo ukawapa falme na taifa za watu, ulizowagawia sawasawa na mafungu yao; hivyo wakaimiliki nchi ya Sihoni, naam, nchi yake mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu, mfalme wa Bashani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ukawaruhusu kushinda falme na mataifa, ukawafanyia mengi kila upande. Wakaishinda nchi ya Heshboni alikotawala mfalme Sihoni; na tena wakaishinda nchi ya Bashani alikotawala mfalme Ogu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukawapa nchi za kifalme pamoja na watu wao, ukawagawia nchi huko na huko, ziwe mafungu yao, wakaichukua nchi ya Sihoni na nchi ya mfalme wa Hesiboni na nchi ya Ogi, mfalme wa Basani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pamoja na hayo ukawapa falme na taifa za watu, ulizowagawia sawasawa na mafungu yao; hivyo wakaimiliki nchi ya Sihoni, naam, nchi yake mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu, mfalme wa Bashani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukawapatia ushindi juu ya falme na mataifa, ukawafanyia mengi kila upande. Wakashinda inchi ya Hesiboni iliyotawaliwa na mufalme Sihoni; na tena wakashinda inchi ya Basani iliyotawaliwa na mufalme Ogi.