Nehemiah 9:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hawakuwa waaminifu kwako. Wakakuasi, wakaiacha sheria yako na kuwaua manabii waliowaonya ili wakurudie wewe. Wakakufuru sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini hawakukutii nao wakaasi dhidi yako, wakatupa sheria zako nyuma yao. Wakawaua manabii wako, waliowaonya ili wakurudie, na wakakufuru sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako walioshuhudu juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hawakuwa waaminifu kwako. Wakakuasi, wakaiacha sheria yako na kuwaua manabii waliowaonya ili wakurudie wewe. Wakakufuru sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini hawakukutii nao wakaasi dhidi yako, wakatupa sheria zako nyuma yao. Wakawaua manabii wako, waliowaonya ili wakurudie, wakafanya makufuru makubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini hawakukutii nao wakaasi dhidi yako, wakatupa sheria zako nyuma yao. Wakawaua manabii wako, waliowaonya ili wakurudie, na wakafanya makufuru makubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hawakuwa waaminifu kwako. Wakakuasi, wakaiacha sheria yako na kuwaua manabii waliowaonya ili wakurudie wewe. Wakakufuru sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wakakataa kutii, wakakuinukia, wakayatupa Maonyo yako nyuma yao, nao wafumbuaji wako wakawaua, kwa kuwa waliwaumbua kwa ushuhuda wao, wawarudishe kwako, wakasema masimango makuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako walioshuhudu juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hawakukuwa waaminifu kwako. Wakakuasi, wakaacha sheria yako na kuwaua manabii waliowaonya kusudi wakurudilie wewe. Wakatenda zambi kubwa mbele yako.