Nehemiah 9:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, ukawatia katika mikono ya adui zao, nao wakawatesa. Lakini wakiwa katika mateso yao, wakakulilia, nawe ukawasikia kutoka mbinguni. Na kwa huruma zako nyingi, ukawapelekea viongozi wa kuwaokoa; nao wakawakomboa toka mikononi mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo ukawatia mikononi mwa adui zao, ambao waliwatesa. Lakini walipoteswa, wakakulilia wewe. Uliwasikia ukiwa mbinguni, nawe kwa huruma zako kuu ukawapa wakombozi, waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa katika mikono ya adui zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, ukawatia katika mikono ya adui zao, nao wakawatesa. Lakini wakiwa katika mateso yao, wakakulilia, nawe ukawasikia kutoka mbinguni. Na kwa huruma zako nyingi, ukawapelekea viongozi wa kuwaokoa; nao wakawakomboa toka mikononi mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo ukawatia mikononi mwa adui zao, ambao waliwatesa. Lakini walipoteswa wakakulilia wewe. Kutoka mbinguni uliwasikia, nawe kwa huruma zako kuu ukawapa waokozi, waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo ukawatia mikononi mwa adui zao, ambao waliwatesa. Lakini walipoteswa, wakakulilia wewe. Kutoka mbinguni uliwasikia, nawe kwa huruma zako kuu ukawapa waokozi, waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, ukawatia katika mikono ya adui zao, nao wakawatesa. Lakini wakiwa katika mateso yao, wakakulilia, nawe ukawasikia kutoka mbinguni. Na kwa huruma zako nyingi, ukawapelekea viongozi wa kuwaokoa; nao wakawakomboa toka mikononi mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo ukawatoa na kuwatia mikononi mwao waliowasonga, wakawasonga kweli; lakini hizo siku za kusongeka kwao walipokulilia, ukawasikia toka mbinguni, tena kwa huruma zako nyingi ukawapatia waokozi, wakawaokoa mikononi mwao waliowasonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa katika mikono ya adui zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, ukawatia katika mikono ya waadui zao, nao wakawatesa. Lakini wakiwa katika mateso yao, wakakulilia, nawe ukawasikiliza kutoka mbinguni. Na kwa rehema zako nyingi, ukawatumia viongozi wa kuwaokoa; nao wakawakomboa toka katika mikono yao.