Nehemiah 9:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukawaonya ili wairudie sheria yako. Hata hivyo, kwa kiburi chao, wakaacha kuzitii amri zako. Wakayaasi maagizo yako, ambayo kwayo mtu akiyatii, ataishi. Wakawa wajeuri pia wakafanya shingo zao ngumu, na wakakataa kuwa watiifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari, wasizisikilize amri zako, bali wakazihalifu hukumu zako, (ambazo mtu akizitenda ataishi katika hizo), nao wakayaondoa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukawaonya ili wairudie sheria yako. Hata hivyo, kwa kiburi chao, wakaacha kuzitii amri zako. Wakayaasi maagizo yako, ambayo kwayo mtu akiyatii, ataishi. Wakawa wajeuri pia wakafanya shingo zao ngumu, na wakakataa kuwa watiifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari, wasizisikilize amri zako, bali wakayaasi maagizo yako, (ambazo mtu akizitenda ataishi katika hizo), nao wakayaondoa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukawaonya ili wairudie sheria yako. Hata hivyo, kwa kiburi chao, wakaacha kuzitii amri zako. Wakayaasi maagizo yako, ambayo kwayo mtu akiyatii, ataishi. Wakawa wajeuri pia wakafanya shingo zao ngumu, na wakakataa kuwa watiifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe ukawaumbua kwa ushuhuda wako, upate kuwarudisha, wayafuate Maonyo yako, lakini wao wakajikuza, hawakuyasikia maagizo yako, nayo maamuzi yako wakayakosea, tena mtu akiyafanya hujipatia kuishi. Wakakutolea mabega makatavu, nazo kosi zao wakazishupaza, hawakusikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari, wasizisikilize amri zako, bali wakazihalifu hukumu zako, (ambazo mtu akizitenda ataishi katika hizo), nao wakayaondoa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukawaonya kusudi warudilie Sheria yako, hata hivyo, kwa kiburi chao, wakaacha kutii amri zako. Wakaasi maagizo yako, ambayo kwa njia yake mutu akiyatii, ataishi. Wakakuwa wenye kiburi vilevile wakakuwa wagumu, na wakakataa kuwa watiifu.