Nehemiah 9:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma katika kile Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, kwa muda wa robo siku, na wakatumia robo nyingine kwa kuungama dhambi na kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha torati ya Bwana, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama, wakamwabudu Bwana, Mungu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria ya BWANA Mungu wao kwa muda wa robo siku, wakatumia robo nyingine kwa kuungama na kumwabudu BWANA Mungu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Torati ya bwana Mwenyezi Mungu wao kwa muda wa robo siku, na wakatumia robo nyingine kwa kuungama dhambi na kumwabudu bwana Mwenyezi Mungu wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha Torati ya BWANA, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama na kumwabudu BWANA, Mungu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakainuka, wasimame hapohapo, walipokuwa, wakasoma katika kitabu cha Maonyo ya Bwana Mungu wao saa tatu, saa tatu nyingine wakaungama na kumwangukia Bwana Mungu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha torati ya BWANA, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama, wakamwabudu BWANA, Mungu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa muda wa yapata saa tatu, walisimama wakati Sheria ya Yawe, Mungu wao, ikisomwa. Na kwa saa tatu zilizofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Yawe, Mungu wao.