Nehemiah 9:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawakukutumikia katika ufalme wao, wala walipoyafurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi, katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa hawakuyaacha matendo yao maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata walipokuwa wangali katika ufalme wao, wakiufurahia wema wako mkuu katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa, hawakukutumikia wala kugeuka kutoka njia zao mbaya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika ufalme wao, na katika wema wako mkuu uliowapa, na katika nchi ile kubwa yenye neema uliyowapa mbele yao, wala hawakughairi na kuyaacha mabaya yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawakukutumikia katika ufalme wao, wala walipoyafurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi, katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa hawakuyaacha matendo yao maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata walipokuwa wangali katika ufalme wao, wakiufurahia wema wako mkuu katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa, hawakukutumikia wala kugeuka kutoka katika njia zao mbaya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata walipokuwa wangali katika ufalme wao, wakiufurahia wema wako mkuu katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa, hawakukutumikia wala kugeuka kutoka njia zao mbaya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika ufalme wao, na katika wema wako mkuu uliowapa, na katika nchi ile kubwa yenye neema uliyowapa mbele yao, wala hawakubadili nia na kuyaacha mabaya yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawakukutumikia katika ufalme wao, wala walipoyafurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi, katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa hawakuyaacha matendo yao maovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ijapo uliwapa ufalme wao, ukawatolea wema wako mwingi, ukawapa nchi kubwa yenye vinono, waione na macho yao, lakini wao hawakukutumikia, wala hawakurudi na kuyaacha matendo yao mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika ufalme wao, na katika wema wako mkuu uliowapa, na katika nchi ile kubwa yenye neema uliyowapa mbele yao, wala hawakughairi na kuyaacha mabaya yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawakukutumikia katika ufalme wao, wala walipofurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi, katika inchi kubwa na yenye mboleo uliyowapa hawakuyaacha matendo yao maovu.