Nehemiah 9:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na leo tumekuwa watumwa; tu watumwa katika nchi uliyowapa babu zetu wafurahie matunda na vipawa vyake vyema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini tazama, sisi ni watumwa leo, watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu ili wapate kula matunda yake na vitu vingine vizuri inayozalisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, sisi hapa tu watumwa leo, na katika habari ya nchi hii uliyowapa baba zetu, wapate kula matunda yake na mema yake, tazama, sisi hapa tu watumwa ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na leo tumekuwa watumwa; tu watumwa katika nchi uliyowapa babu zetu wafurahie matunda na vipawa vyake vyema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini tazama, leo sisi ni watumwa, watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu ili wapate kula matunda yake na vitu vingine vizuri inayozalisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini tazama, sisi ni watumwa leo, watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu ili wapate kula matunda yake na vitu vingine vizuri inayozalisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, sisi hapa tu watumwa leo, na katika nchi hii uliyowapa baba zetu, wapate kula matunda yake na mema yake, tazama, sisi hapa tu watumwa ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na leo tumekuwa watumwa; tu watumwa katika nchi uliyowapa babu zetu wafurahie matunda na vipawa vyake vyema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo sisi tu watumwa katika nchi, uliyowapa baba zetu, wayale mazao yake na mema yake, tazama, kuku huku sisi tu watumwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, sisi hapa tu watumwa leo, na katika habari ya nchi hii uliyowapa baba zetu, wapate kula matunda yake na mema yake, tazama, sisi hapa tu watumwa ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na leo tumekuwa watumwa; tuko watumwa katika inchi uliyowapa babu zetu kwa kufurahia matunda yake na mazao yake mema.