Numbers 10:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale waliokuwa chini ya bendera ya kikosi cha kabila la Yuda, walitangulia, kundi moja baada ya jingine. Kiongozi wao alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya beramu yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mahali pa mbele ilisafiri beramu ya marago ya wana wa Yuda, kwa majeshi yao; na Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyekuwa juu ya jeshi lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale waliokuwa chini ya bendera ya kikosi cha kabila la Yuda, walitangulia, kundi moja baada ya jingine. Kiongozi wao alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nahshoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mahali pa mbele ilisafiri beramu ya kambi ya wana wa Yuda, kwa majeshi yao; na Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyekuwa juu ya jeshi lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale waliokuwa chini ya bendera ya kikosi cha kabila la Yuda, walitangulia, kundi moja baada ya jingine. Kiongozi wao alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwanza ikaondoka bendera ya makambi ya wana wa Yuda, vikosi kwa vikosi, naye mkuu wa vikosi vyao alikuwa Nasoni, mwana wa Aminadabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mahali pa mbele ilisafiri beramu ya marago ya wana wa Yuda, kwa majeshi yao; na Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyekuwa juu ya jeshi lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale waliokuwa chini ya bendera ya jeshi la kabila la Yuda, wakatangulia, kundi moja kisha lingine. Kiongozi wao alikuwa Nasoni mwana wa Aminadabu.