Numbers 10:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wakati wa vita nchini mwenu dhidi ya adui wanaowashambulia, mtatoa ishara ya vita kwa kupiga tarumbeta hizi ili Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu apate kuwakumbuka na kuwaokoa na adui zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuokolewa kutoka kwa adui zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wakati wa vita nchini mwenu dhidi ya adui wanaowashambulia, mtatoa ishara ya vita kwa kupiga tarumbeta hizi ili Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu apate kuwakumbuka na kuwaokoa na adui zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa na BWANA Mungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa na bwana Mwenyezi Mungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wakati wa vita nchini mwenu dhidi ya adui wanaowashambulia, mtatoa ishara ya vita kwa kupiga tarumbeta hizi ili Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu apate kuwakumbuka na kuwaokoa na adui zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo, mtakapokwenda vitani katika nchi yenu kupigana na adui watakaowasonga, na mshangilie na kuyapiga hayo matarumbeta; ndipo, mtakapokumbukwa mbele ya Bwana Mungu wenu, mwokolewe katika adui zenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa vita katika inchi yenu juu ya waadui wanaowashambulia, mutatoa kitambulisho cha vita kwa kupiga baragumu hizi kusudi Yawe, Mungu wenu apate kuwakumbuka na kuwaokoa na waadui zenu.