Numbers 11:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu walianza kumlalamikia Mwenyezi-Mungu juu ya taabu zao. Mwenyezi-Mungu aliposikia, alishikwa na hasira, akawapelekea moto. Moto huo uliwaka kati yao na kuchoma upande mmoja wa kambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Mwenyezi Mungu, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Mwenyezi Mungu ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa Bwana; Bwana aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa Bwana ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu walianza kumlalamikia Mwenyezi-Mungu juu ya taabu zao. Mwenyezi-Mungu aliposikia, alishikwa na hasira, akawapelekea moto. Moto huo uliwaka kati yao na kuchoma upande mmoja wa kambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa BWANA, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa BWANA ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu walianza kumlalamikia Mwenyezi-Mungu juu ya taabu zao. Mwenyezi-Mungu aliposikia, alishikwa na hasira, akawapelekea moto. Moto huo uliwaka kati yao na kuchoma upande mmoja wa kambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu wakanuna, vikawa vibaya masikioni mwa Bwana; naye Bwana alipovisikia, makali yake yakawaka moto, nao moto wa Bwana ukawawakia, ukayala makambi yaliyokuwa pembeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha hao watu walikuwa kama wanung’unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wakaanza kunungunika mbele ya Yawe juu ya taabu zao. Yawe akasikia, na hasira yake ikawaka. Moto toka kwa Yawe ukawaka kati yao na kuchoma upande mumoja wa kambi.