Numbers 11:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali kwa muda wa mwezi mzima! Mtaila hadi iwatoke puani, mpaka muikinai. Yote hayo ni kwa sababu mmemkataa Mwenyezi-Mungu aliye hapahapa miongoni mwenu, na kulia mbele yake mkisema, ‘Kwa nini tulitoka Misri?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bali kwa mwezi mzima hadi iwatokee puani, nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataa Mwenyezi Mungu, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa Bwana aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali kwa muda wa mwezi mzima! Mtaila hadi iwatoke puani, mpaka muikinai. Yote hayo ni kwa sababu mmemkataa Mwenyezi-Mungu aliye hapahapa miongoni mwenu, na kulia mbele yake mkisema, ‘Kwa nini tulitoka Misri?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bali kwa mwezi mzima mpaka ziwatokee puani nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataa BWANA, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bali kwa mwezi mzima mpaka iwatokee puani, nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataa bwana, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hadi hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa BWANA aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali kwa muda wa mwezi mzima! Mtaila hadi iwatoke puani, mpaka muikinai. Yote hayo ni kwa sababu mmemkataa Mwenyezi-Mungu aliye hapahapa miongoni mwenu, na kulia mbele yake mkisema, ‘Kwa nini tulitoka Misri?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila na mzile mwezi mzima, hata zitoke puani mwenu, hata ziwatapishe, kwa kuwa mmemkataa Bwana anayekaa katikati yenu, mlipomlilia kwamba: Kwa nini tumetoka Misri?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa BWANA aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini kwa muda wa mwezi muzima! Mutaikula mpaka iwatoke ndani ya pua, mpaka muichukie. Yote hayo ni kwa sababu mumemukataa Yawe anayekuwa hapahapa kati yenu, na kulia mbele yake mukisema: Kwa nini tulitoka Misri?