Numbers 11:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Je, uwezo wangu umepungua? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au la.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akamjibu Musa, “Je, mkono wa Mwenyezi Mungu ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Musa, Je! Mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Je, uwezo wangu umepungua? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au la.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akamjibu Mose, “Je, mkono wa BWANA ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema halitatimizwa kwa ajili yako au la.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akamjibu Musa, “Je, mkono wa bwana ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Musa, Je! Mkono wa BWANA umepungua urefu wake? Sasa utaona kama neno langu litatimizwa kwako, au la.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Je, uwezo wangu umepungua? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au la.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Je? Mkono wa Bwana umegeuka kuwa mfupi? Sasa utaona, kama neno langu linakupatia kitu, au kama ni la bure.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Musa, Je! Mkono wa BWANA umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamujibu Musa: Uwezo wangu umepunguka? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au hapana.