Numbers 12:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wingu lilipoondoka juu ya hema la mkutano, Miriamu alionekana ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni alipogeuka na kumtazama Miriamu, alishangaa kuona kuwa ameshikwa na ukoma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hilo wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Haruni akamgeukia, akaona ana ukoma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wingu lilipoondoka juu ya hema la mkutano, Miriamu alionekana ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni alipogeuka na kumtazama Miriamu, alishangaa kuona kuwa ameshikwa na ukoma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati hilo wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia akaona ana ukoma;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Haruni akamgeukia, akaona ana ukoma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na kumwona akiwa mwenye ukoma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wingu lilipoondoka juu ya hema la mkutano, Miriamu alionekana ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni alipogeuka na kumtazama Miriamu, alishangaa kuona kuwa ameshikwa na ukoma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nalo wingu likaondoka juu ya Hema; walipotazama, Miriamu alikuwa mwenye ukoma uliokuwa mweupe kama chokaa juani. Haroni naye alipomgeukia Miriamu akamwona, ya kuwa ni mwenye ukoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wingu lilipoondoka juu ya hema la mukutano, Miriamu akaonekana yuko na ukoma, mweupe kama teluji. Haruni alipogeuka na kumwangalia Miriamu, akashangaa kuona kwamba ameshikwa na ukoma.