Numbers 12:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Mwenyezi-Mungu akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye mlango wa hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wote wawili wakasogea mbele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Haruni na Miriamu. Waliposogea mbele,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Mwenyezi-Mungu akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye mlango wa hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wote wawili wakasogea mbele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Haruni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Mwenyezi-Mungu akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye mlango wa hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wote wawili wakasogea mbele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akashuka katika lile wingu lililokuwa kama nguzo, akasimama hapo pa kuliingilia Hema, akamwita Haroni na Miriamu, nao wakatokea wote wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo Yawe akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye mulango wa hema, akawaita Haruni na Miriamu. Wote wawili wakasogea mbele.