Numbers 12:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi huongea naye ana kwa ana, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye huliona umbo langu mimi Mwenyezi-Mungu. Kwa nini, basi, hamkuogopa kusema vibaya dhidi ya mtumishi wangu Mose?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwake nitanena naye uso kwa uso, waziwazi wala si kwa mafumbo; yeye ataona umbo la Mwenyezi Mungu. Kwa nini basi ninyi hamkuogopa kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Musa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi huongea naye ana kwa ana, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye huliona umbo langu mimi Mwenyezi-Mungu. Kwa nini, basi, hamkuogopa kusema vibaya dhidi ya mtumishi wangu Mose?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwake nitanena naye uso kwa uso, waziwazi wala si kwa mafumbo; yeye ataona umbo la BWANA. Kwa nini basi ninyi hamkuogopa kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwake nitanena naye uso kwa uso, waziwazi wala si kwa mafumbo; yeye ataona umbo la bwana. Kwa nini basi ninyi hamkuogopa kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Musa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi huongea naye ana kwa ana, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye huliona umbo langu mimi Mwenyezi-Mungu. Kwa nini, basi, hamkuogopa kusema vibaya dhidi ya mtumishi wangu Mose?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nasema naye kinywa kwa kinywa, naye huniona mimi Bwana, nilivyo, haoni kivulivuli tu au mfano tu; kwa nini ninyi hamkuogopa kuteta na mtumishi wangu Mose?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ninaongea naye kinywa kwa kinywa, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye ameliona umbo langu mimi Yawe. Kwa nini, basi, hamukuogopa kusema vibaya juu ya mutumishi wangu Musa?