Numbers 14:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliwalalamikia Mose na Aroni wakisema, “Afadhali tungefia Misri! Afadhali tungefia papa hapa jangwani!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Musa na Haruni, na kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliwalalamikia Mose na Aroni wakisema, “Afadhali tungefia Misri! Afadhali tungefia papa hapa jangwani!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wote wakanung'unika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Musa na Haruni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wana wa Israeli wote wakawanung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliwalalamikia Mose na Aroni wakisema, “Afadhali tungefia Misri! Afadhali tungefia papa hapa jangwani!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wote wa Isiraeli wakamnung'unikia Mose na Haroni, nao wote walio wa mkutano wao wakawaambia: Afadhali tungalikufa katika nchi ya Misri au tungekufa huku nyikani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamunungunikia Musa na Haruni wakisema: Afazali tungekufia Misri! Afazali tungekufia hapahapa katika jangwa!