Numbers 14:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenungunika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenung’unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenung'unika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na ambaye amenung'unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenung’unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenungunika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huku nyikani itaanguka mizoga yenu ninyi nyote mliokaguliwa na kuhesabiwa, mlio wenye miaka ishirini na zaidi, mlioninung'unikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung’unikia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakufa na miili yenu itatupwa humuhumu katika jangwa, kwa sababu mumenungunika juu yangu, hakuna hata mumoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka makumi mbili na zaidi,