Numbers 14:40 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake, waliamka alfajiri na mapema wakaenda sehemu za milimani, wakisema, “Sasa tuko tayari kabisa kwenda mahali ambapo Mwenyezi-Mungu alituahidi. Tunakiri kwamba tulitenda dhambi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi na mapema siku iliyofuata, walipanda kilele kirefu cha nchi ya vilima, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea hadi mahali Mwenyezi Mungu alipotuahidi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali Bwana alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake, waliamka alfajiri na mapema wakaenda sehemu za milimani, wakisema, “Sasa tuko tayari kabisa kwenda mahali ambapo Mwenyezi-Mungu alituahidi. Tunakiri kwamba tulitenda dhambi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahali BWANA alipotuahidi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahali bwana alipotuahidi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake, waliamka alfajiri na mapema wakaenda sehemu za milimani, wakisema, “Sasa tuko tayari kabisa kwenda mahali ambapo Mwenyezi-Mungu alituahidi. Tunakiri kwamba tulitenda dhambi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake wakaamka na mapema, wakapanda mlimani juu kileleni na kusema: Basi, tumekwisha kufika huku, sasa twende kupanda mahali pale, Bwana alipotuelekeza! Kwani tumekosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake, wakaamuka asubui mapema wakaenda sehemu za milima, wakisema: Sasa tuko tayari kabisa kwenda pahali ambapo Yawe alituahidi. Tunaitika kwamba tulitenda zambi.