Numbers 14:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mradi tu msimwasi Mwenyezi-Mungu, wala msiwaogope wenyeji wa nchi hiyo. Maana wao ni mboga tu kwetu; kinga yao imekwisha ondolewa kwao, naye Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi; msiwaogope!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ila tu msimwasi Mwenyezi Mungu. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi. Msiwaogope.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mradi tu msimwasi Mwenyezi-Mungu, wala msiwaogope wenyeji wa nchi hiyo. Maana wao ni mboga tu kwetu; kinga yao imekwisha ondolewa kwao, naye Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi; msiwaogope!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ila tu msimwasi BWANA. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini BWANA yupo pamoja nasi. Msiwaogope.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ila tu msimwasi bwana. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini bwana yupo pamoja nasi. Msiwaogope.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mradi tu msimwasi Mwenyezi-Mungu, wala msiwaogope wenyeji wa nchi hiyo. Maana wao ni mboga tu kwetu; kinga yao imekwisha ondolewa kwao, naye Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi; msiwaogope!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni hili tu, msimpingie Bwana! Tena wale watu wa nchi hiyo msiwaogope, kwani watakuwa kama chakula chetu, nacho kivuli, walichokikimbilia, kimeondoka kwao, naye Bwana yuko pamoja na sisi, kwa hiyo msiwaogope!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini musimwasi tu Yawe, wala musiwaogope wenyeji wa inchi hiyo. Maana wao ni kama mboga tu kwetu. Kingo yao imekwisha kuondolewa kwao naye Yawe yuko pamoja nasi. Musiwaogope!