Numbers 15:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kama kuna mgeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au daima, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atafanya kama mnavyofanya nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa vizazi vijavyo, wakati wowote mgeni au mtu mwingine yeyote anayeishi miongoni mwenu aletapo sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu, ni lazima afanye sawasawa kabisa na jinsi mnavyofanya ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kwamba mgeni amekaa kwenu, au mtu ye yote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye yuataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa Bwana; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kama kuna mgeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au daima, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atafanya kama mnavyofanya nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa vizazi vijavyo, wakati wo wote mgeni au mtu mwingine ye yote anayeishi miongoni mwenu aletapo sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kumpendeza BWANA, ni lazima afanye sawasawa kabisa na jinsi mnavyofanya ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa vizazi vijavyo, wakati wowote mgeni au mtu mwingine yeyote anayeishi miongoni mwenu aletapo sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kumpendeza bwana, ni lazima afanye sawasawa kabisa na jinsi mnavyofanya ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ikiwa mgeni amekaa kwenu, au mtu yeyote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye anataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa BWANA; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kama kuna mgeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au daima, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atafanya kama mnavyofanya nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama kwenu yuko mgeni au mwingine anayekaa siku zote kwao walio vizazi vyenu, naye akitaka kumtengenezea Bwana ng'ombe ya tambiko kuwa mnuko wa moto wa kumpendeza, na aitengeneze vivyo hivyo, kama ninyi mnavyoitengeneza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kwamba mgeni amekaa kwenu, au mtu ye yote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye yuataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa BWANA; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama kuna mugeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au siku zote, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza kwa moto, harufu inayomupendeza Yawe, mutu huyo atafanya kama vile munavyofanya ninyi.