Numbers 15:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, ikiwa kosa hilo limefanyika bila kukusudia, bila jumuiya kujua, jumuiya yote itatoa fahali mmoja mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu, pamoja na sadaka yake ya nafaka na ya divai kufuatana na maagizo yake. Kadhalika watu watatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ikiwa hili limefanyika pasipo kukusudia bila jumuiya kuwa na habari nalo, basi jumuiya yote itatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa ikiwa harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu, pamoja na sadaka ya nafaka na ya kinywaji zilizoamriwa kwayo, na beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo itakapokuwa, kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu, ndipo mkutano wote utasongeza ng'ombe mume mmoja mdogo kuwa sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana, pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji, kama amri ilivyo, na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, ikiwa kosa hilo limefanyika bila kukusudia, bila jumuiya kujua, jumuiya yote itatoa fahali mmoja mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu, pamoja na sadaka yake ya nafaka na ya divai kufuatana na maagizo yake. Kadhalika watu watatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ikiwa hili limefanyika pasipo kukusudia bila jumuiya kuwa na habari nalo, basi jumuiya yote itatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa ikiwa harufu nzuri inayompendeza BWANA, pamoja na sadaka ya nafaka na ya kinywaji zilizoamriwa kwayo, na mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ikiwa hili limefanyika pasipo kukusudia bila jumuiya kuwa na habari nalo, basi jumuiya yote itatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa ikiwa harufu nzuri inayompendeza bwana, pamoja na sadaka ya nafaka na ya kinywaji zilizoamriwa kwayo, na mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo itakapokuwa, kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu, ndipo mkutano wote utasongeza ng'ombe dume mdogo mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA, pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji, kama amri ilivyo, na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi, ikiwa kosa hilo limefanyika bila kukusudia, bila jumuiya kujua, jumuiya yote itatoa fahali mmoja mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu, pamoja na sadaka yake ya nafaka na ya divai kufuatana na maagizo yake. Kadhalika watu watatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama ni makosa yaliyofanyika kwa kupotelewa tu, ikiwa wao wa mkutano hawakuyaona, basi, mkutano wote na utengeneze dume moja la ng'ombe aliye kijana bado kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima kuwa mnuko wa kumpendeza Bwana; waitoe pamoja na kilaji na kinywaji chake cha tambiko, kama ilivyo desturi, tena watoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo itakapokuwa, kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu, ndipo mkutano wote utasongeza ng’ombe mume mmoja mdogo kuwa sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA, pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji, kama amri ilivyo, na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, ikiwa kosa hilo limefanyika bila kukusudia, bila Waisraeli wote pamoja kujua, watatoa mwana-ngombe dume mumoja kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumupendeza Yawe, pamoja na sadaka yake ya vyakula na ya kinywaji kufuatana na maagizo yake. Vilevile watu watatoa beberu mumoja kuwa sadaka kwa ajili ya zambi.