Numbers 15:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atafanya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya huyo mtu aliyekosa bila kujua, naye atasamehewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atafanya upatanisho mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya yule aliyekosa kwa kufanya dhambi pasipo kukusudia, upatanisho utakapofanywa kwa ajili yake, atasamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi pasipo kujua, mbele za Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasemehewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atafanya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya huyo mtu aliyekosa bila kujua, naye atasamehewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atafanya upatanisho mbele za BWANA kwa ajili ya yule aliyekosa kwa kufanya dhambi pasipo kukusudia, wakati upatanisho utakapokuwa umefanyika kwa ajili yake, atasamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atafanya upatanisho mbele za bwana kwa ajili ya yule aliyekosa kwa kufanya dhambi pasipo kukusudia, upatanisho utakapofanywa kwa ajili yake, atasamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi pasipo kujua, mbele za BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasamehewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atafanya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya huyo mtu aliyekosa bila kujua, naye atasamehewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji na ampatie upozi mtu huyo aliyepotelewa, akitoa mbele ya Bwana ng'ombe ya tambiko ya kumweua kwa ajili ya kupotelewa kwake; akimpatia upozi hivyo, ataondolewa kosa lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi pasipo kujua, mbele za BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasemehewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atafanya upatanisho mbele ya Yawe, kwa ajili ya huyo mutu aliyekosa bila kujua, naye atasamehewa.