Numbers 15:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtafuata sheria moja kila mtu atakayekosea bila kukusudia, awe ni mwananchi Mwisraeli au ni mgeni anayeishi pamoja nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sheria hiyo moja itamhusu kila mmoja ambaye ametenda dhambi pasipo kukusudia, awe Mwisraeli mzawa ama mgeni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtafuata sheria moja kila mtu atakayekosea bila kukusudia, awe ni mwananchi Mwisraeli au ni mgeni anayeishi pamoja nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sheria hiyo moja itamhusu kila mmoja ambaye ametenda dhambi pasipo kukusudia, awe mzawa ama mgeni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sheria hiyo moja itamhusu kila mmoja ambaye ametenda dhambi pasipo kukusudia, awe Mwisraeli mzawa ama mgeni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtafuata sheria moja kila mtu atakayekosea bila kukusudia, awe ni mwananchi Mwisraeli au ni mgeni anayeishi pamoja nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ni mwenyeji wa wana wa Isiraeli, au kama ni mgeni atakayekaa ugenini kwenu, maongozi yawe yayo hayo ya kuwafanyizia waliokosa kwa kupotelewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutafuata sheria moja kila mutu atakayekosa bila kukusudia, akuwe ni mwanainchi Mwisraeli au ni mugeni anayeishi pamoja nanyi.