Numbers 15:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vishada hivyo vitakuwa kumbukumbu kwenu. Kila mtakapoviona, mtazikumbuka amri zangu zote na kuzifuata, ili msije mkafuata matakwa yenu na yale mnayoyaona kwa macho yenu wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakuwa mkivitazama vifundo hivyo ili mpate kukumbuka amri zote za Mwenyezi Mungu, ili mpate kuzitii msije mkajitia uzinzi wenyewe kwa kuzifuata tamaa za mioyo yenu na za macho yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya Bwana, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vishada hivyo vitakuwa kumbukumbu kwenu. Kila mtakapoviona, mtazikumbuka amri zangu zote na kuzifuata, ili msije mkafuata matakwa yenu na yale mnayoyaona kwa macho yenu wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtakuwa mkivitazama vifundo hivyo ili mpate kukumbuka amri zote za BWANA, ili mpate kuzitii msije mkajitia uzinzi wenyewe kwa kuzifuata tamaa za mioyo yenu na za macho yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtakuwa mkivitazama vifundo hivyo ili mpate kukumbuka amri zote za bwana, ili mpate kuzitii msije mkajitia uzinzi wenyewe kwa kuzifuata tamaa za mioyo yenu na za macho yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya BWANA, na kuyafanya; tena ili msiende kutangatanga kufuata mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vishada hivyo vitakuwa kumbukumbu kwenu. Kila mtakapoviona, mtazikumbuka amri zangu zote na kuzifuata, ili msije mkafuata matakwa yenu na yale mnayoyaona kwa macho yenu wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana ya hivyo vishada vyenu ni hii: mtakapoviona, myakumbuke maagizo yote ya Bwana, myafanye, msizifuate tamaa za mioyo yenu na za macho yenu, kwani mkizifuata hufanya ugoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya BWANA, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vishada hivyo vitakuwa ukumbusho kwenu. Kila mara mutakapoviona, mutakumbuka amri zangu zote na kuzifuata, kusudi musifuate mapenzi yenu na yale munayoona kwa macho yenu wenyewe.