Numbers 16:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Kora akawakusanya watu wote pamoja, wakasimama mbele ya Mose na Aroni ambao walikuwa mlangoni mwa hema la mkutano. Ndipo utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukawatokea watu wote!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Musa na Haruni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa Mwenyezi Mungu ukatokea kwa kusanyiko lote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa Bwana ukatokea mbele ya mkutano wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Kora akawakusanya watu wote pamoja, wakasimama mbele ya Mose na Aroni ambao walikuwa mlangoni mwa hema la mkutano. Ndipo utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukawatokea watu wote!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa BWANA ukatokea kwa kusanyiko lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Musa na Haruni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa bwana ukatokea kwa kusanyiko lote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa BWANA ukatokea mbele ya mkutano wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Kora akawakusanya watu wote pamoja, wakasimama mbele ya Mose na Aroni ambao walikuwa mlangoni mwa hema la mkutano. Ndipo utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukawatokea watu wote!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Kora alikuwa aliwakusanya hao wa mkutano wote hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; ndipo, utukufu wa Bwana ulipoutokea huo mkutano wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa BWANA ukatokea mbele ya mkutano wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Kora akawakusanya watu wote pamoja, wakasimama mbele ya Musa na Haruni ambao walikuwa kwenye mulango wa hema la mukutano. Halafu utukufu wa Yawe ukawatokea watu wote.