Numbers 16:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wakaondoka kwenye makao ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu wakatoka mahemani mwao na kusimama mlangoni wakiandamana na wake zao na watoto wao wote hata wale wanaonyonya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wakaondoka kwenye makao ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu wakatoka mahemani mwao na kusimama mlangoni wakiandamana na wake zao na watoto wao wote hata wale wanaonyonya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao akina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wakaondoka kwenye makao ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu wakatoka mahemani mwao na kusimama mlangoni wakiandamana na wake zao na watoto wao wote hata wale wanaonyonya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipoepuka po pote palipoyazunguka makao ya Kora na ya Datani na ya Abiramu, lakini Datani na Abiramu wakatoka, wakasimama hapo pa kuyaingilia mahema yao pamoja na wake zao na wana wao na watoto wao wachanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wakaondoka kwenye makao ya Kora, Datani na Abiramu. Datani na Abiramu wakatoka katika mahema yao na kusimama kwenye mulango wakiandamana na wake zao na watoto wao wote hata wale wanaonyonya.