Numbers 16:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikusanyika mbele ya Mose na Aroni, wakawaambia, “Nyinyi mmepita kikomo! Jumuiya yote ni takatifu na kila mtu katika jumuiya hii ni mtakatifu, na Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi sote. Mbona sasa nyinyi mnajifanya wakuu wa jumuiya ya Mwenyezi-Mungu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaja kama kikundi kuwapinga Musa na Haruni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili wote ni watakatifu, kila mmoja wao, naye Mwenyezi Mungu yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la Mwenyezi Mungu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; n'nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikusanyika mbele ya Mose na Aroni, wakawaambia, “Nyinyi mmepita kikomo! Jumuiya yote ni takatifu na kila mtu katika jumuiya hii ni mtakatifu, na Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi sote. Mbona sasa nyinyi mnajifanya wakuu wa jumuiya ya Mwenyezi-Mungu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaja kama kikundi kuwapinga Mose na Aroni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, naye BWANA yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la BWANA?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaja kama kikundi kuwapinga Musa na Haruni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, naye bwana yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la bwana?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yuko kati yao; ya nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikusanyika mbele ya Mose na Aroni, wakawaambia, “Nyinyi mmepita kikomo! Jumuiya yote ni takatifu na kila mtu katika jumuiya hii ni mtakatifu, na Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi sote. Mbona sasa nyinyi mnajifanya wakuu wa jumuiya ya Mwenyezi-Mungu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakusanyika kutetana na Mose na Haroni, wakawaambia: Maneno yenu ni mengi, kwani wao wote wa mkutano wetu mzima ni watakatifu, naye Bwana yuko katikati yao. Mbona mnajikweza kuwa wakuu wao wa mkutano wa Bwana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yu kati yao; n’nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakakusanyika mbele ya Musa na Haruni, wakawaambia: Ninyi mumepitisha kipimo! Waisraeli wote pamoja ni watakatifu; kila mumoja ni mutakatifu. Yawe yuko pamoja nasi wote. Mbona sasa ninyi munajifanya wakubwa kushinda watu wengine wa Yawe?