Numbers 16:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mwenyezi-Mungu akifanya jambo ambalo halijapata kutendeka, ardhi ikafunuka na kuwameza watu hawa pamoja na kila kitu chao, wakaenda kuzimu wakiwa hai, basi mtajua kuwa watu hawa wamemdharau Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa Mwenyezi Mungu ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mwenyezi-Mungu akifanya jambo ambalo halijapata kutendeka, ardhi ikafunuka na kuwameza watu hawa pamoja na kila kitu chao, wakaenda kuzimu wakiwa hai, basi mtajua kuwa watu hawa wamemdharau Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa BWANA ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini BWANA akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao wakashuka shimoni wakiwa hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau BWANA
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mwenyezi-Mungu akifanya jambo ambalo halijapata kutendeka, ardhi ikafunuka na kuwameza watu hawa pamoja na kila kitu chao, wakaenda kuzimu wakiwa hai, basi mtajua kuwa watu hawa wamemdharau Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana akiumba jambo jipya, nchi ikiasama na kuwameza wao pamoja navyo vyote vilivyo vyao, washuke kuzimuni wakiwa wazima, ndipo, mtakapotambua, ya kuwa watu hao wamemtukana Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini BWANA akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau BWANA
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe akifanya jambo ambalo halijapata kutendeka, udongo ukifunguka na kuwameza watu hawa pamoja na kila kitu chao, na kwenda kuzimu wakiwa uzima, basi mutajua kwamba watu hawa wamemuzarau Yawe.