Numbers 16:40 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hili lilikuwa onyo kwa Waisraeli kwamba mtu yeyote ambaye si kuhani, yaani asiye wa ukoo wa Aroni asiende madhabahuni kumfukizia Mwenyezi-Mungu ubani. La sivyo ataangamizwa kama Kora na wafuasi wake. Haya yote yalitendeka kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Eleazari kwa njia ya Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwelekeza kupitia Musa. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Haruni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele za Mwenyezi Mungu, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni awaye yote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za Bwana; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama Bwana alivyonena naye, kwa mkono wa Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hili lilikuwa onyo kwa Waisraeli kwamba mtu yeyote ambaye si kuhani, yaani asiye wa ukoo wa Aroni asiende madhabahuni kumfukizia Mwenyezi-Mungu ubani. La sivyo ataangamizwa kama Kora na wafuasi wake. Haya yote yalitendeka kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Eleazari kwa njia ya Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama vile BWANA alivyomwelekeza kupitia Mose. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Aroni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele za BWANA, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama vile bwana alivyomwelekeza kupitia Musa. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Haruni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele za bwana, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni yeyote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za BWANA; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama BWANA alivyonena naye, kwa kupitia kwa Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hili lilikuwa onyo kwa Waisraeli kwamba mtu yeyote ambaye si kuhani, yaani asiye wa ukoo wa Aroni asiende madhabahuni kumfukizia Mwenyezi-Mungu ubani. La sivyo ataangamizwa kama Kora na wafuasi wake. Haya yote yalitendeka kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Eleazari kwa njia ya Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo vikawa ukumbusho wa wana wa Isiraeli, kwa kwamba mtu mgeni asiye wa uzao wa Haroni, asije kuvukiza mavukizo mbele ya Bwana, asipatwe na mambo kama Kora na wenzake, aliowakusanya, maana Bwana alivyomwambia kinywani mwa Mose yalimpata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni awaye yote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za BWANA; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama BWANA alivyonena naye, kwa mkono wa Musa.