Numbers 16:46 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako, kitie moto na kukiweka kando ya madhabahu, kisha ukitie ubani halafu uende nacho haraka kwa watu na kuwafanyia upatanisho. Fanya haraka! Ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imekwisha wafikia na pigo limeanza kuwashambulia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akamwambia Haruni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na tauni imeanza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, wende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu zimetoka kwa Bwana; hiyo tauni imeanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako, kitie moto na kukiweka kando ya madhabahu, kisha ukitie ubani halafu uende nacho haraka kwa watu na kuwafanyia upatanisho. Fanya haraka! Ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imekwisha wafikia na pigo limeanza kuwashambulia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa BWANA, na tauni imeanza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akamwambia Haruni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa bwana, na tauni imeanza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, uende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu imetoka kwa BWANA; hiyo tauni imeanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako, kitie moto na kukiweka kando ya madhabahu, kisha ukitie ubani halafu uende nacho haraka kwa watu na kuwafanyia upatanisho. Fanya haraka! Ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imekwisha wafikia na pigo limeanza kuwashambulia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
naye Mose akamwambia Haroni: Chukua chetezo, utie humo moto wa mezani pa kutambikia, kisha weka mavukizo juu yake, uende upesi kwenye mkutano, uwapatie upozi, kwani makali yamekwisha kutoka kwake Bwana, nalo pigo limekwisha kuwaanzia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, wende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu zimetoka kwa BWANA; hiyo tauni imeanza.