Numbers 18:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Pia, vitu vingine vyote watakavyonitolea Waisraeli kama sadaka za kutikisa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wanao na binti zako kuwa haki yenu milele. Mtu yeyote katika jamaa yako asiye najisi anaweza kula vitu hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hiki pia ni chako: chochote kilichotengwa kutoka matoleo yote ya sadaka za kuinuliwa za Waisraeli. Haya ninakupa wewe, na wanao wa kiume na wa kike kuwa sehemu yenu ya milele. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ametakasika anaweza kuyala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Pia, vitu vingine vyote watakavyonitolea Waisraeli kama sadaka za kutikisa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wanao na binti zako kuwa haki yenu milele. Mtu yeyote katika jamaa yako asiye najisi anaweza kula vitu hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hiki pia ni chako: cho chote kilichotengwa kutoka kwenye matoleo yote ya sadaka za kupunga za Waisraeli. Ninakupa wewe haya, wana na binti zako kama sehemu yenu ya kawaida. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ni safi kwa taratibu za ibada anaweza kuyala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hiki pia ni chako: chochote kilichotengwa kutoka kwenye matoleo yote ya sadaka za kuinuliwa za Waisraeli. Ninakupa wewe haya, wana na binti zako kama sehemu yenu ya kawaida. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ni safi kwa taratibu za ibada anaweza kuyala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Pia, vitu vingine vyote watakavyonitolea Waisraeli kama sadaka za kutikisa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wanao na binti zako kuwa haki yenu milele. Mtu yeyote katika jamaa yako asiye najisi anaweza kula vitu hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena ninakupa wewe na wanao wa kiume na wa kike kuwa vyenu: vipaji vyao vya tambiko, wanavyovitoa vya kunyanyuliwa, navyo vipaji vya tambiko vya wana wa Isiraeli vya kupitishwa motoni viwe vyako; hii na iwe haki yenu ya kale na kale. Kila atakayekuwa nyumbani mwako, akiwa ametakata, na avile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, vitu vingine vyote Waisraeli watakavyonitolea kama vile sadaka za kutikiswa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wana wako na wabinti zako kuwa haki yenu milele. Mutu yeyote katika jamaa yako asiyekuwa muchafu anaweza kula vitu hivyo.