Numbers 18:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli hunitolea: Mafuta safi, divai na nafaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa Mwenyezi Mungu kama malimbuko katika mavuno yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa Bwana, amekupa wewe hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli hunitolea: mafuta safi, divai na nafaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote na divai mpya iliyo bora kuliko zote wanayompa BWANA kama malimbuko katika mavuno yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa bwana kama malimbuko katika mavuno yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, hayo nimekupa wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli hunitolea: Mafuta safi, divai na nafaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mafuta yote yaliyo mazuri mno nazo mvinyo mbichi zilizo nzuri mno nazo ngano, watakazomtolea Bwana za malimbuko, ninakupa wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, amekupa wewe hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli wananitolea: mafuta safi, divai na ngano.