Numbers 18:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mazao yote ya kwanza ya matunda mabivu ya mashamba yao ambayo wataniletea mimi, yatakuwa yako. Kila mtu asiye najisi katika jamaa yako anaweza kula.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamletea Mwenyezi Mungu yatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani mwako ambaye ametakasika anaweza kula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Matunda ya kwanza yaivayo katika yote yaliyo katika nchi yao, watakayomletea Bwana, yatakuwa yako, kila mtu aliye safi katika nyumba yako atakula katika vitu hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mazao yote ya kwanza ya matunda mabivu ya mashamba yao ambayo wataniletea mimi, yatakuwa yako. Kila mtu asiye najisi katika jamaa yako anaweza kula.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamletea BWANA yatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani kwako ambaye ni safi kwa taratibu za Ibada anaweza kula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamletea bwana yatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani kwako ambaye ni safi kwa taratibu za Ibada anaweza kula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Matunda ya kwanza yaivayo katika yote yaliyo katika nchi yao, watakayomletea BWANA, yatakuwa yako, kila mtu aliye safi katika nyumba yako atakula katika vitu hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mazao yote ya kwanza ya matunda mabivu ya mashamba yao ambayo wataniletea mimi, yatakuwa yako. Kila mtu asiye najisi katika jamaa yako anaweza kula.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mazao yote ya kwanza ya nchi yao, watakayomtolea Bwana, yatakuwa yako; kila atakayekuwa nyumbani mwako, akiwa ametakata, na ayale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Matunda ya kwanza yaivayo katika yote yaliyo katika nchi yao, watakayomletea BWANA, yatakuwa yako, kila mtu aliye safi katika nyumba yako atakula katika vitu hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mazao yote ya kwanza ya matunda mabichi ya mashamba yao ambayo wataniletea mimi, yatakuwa yako. Kila mutu asiyekuwa muchafu katika jamaa yako anaweza kula.