Numbers 18:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kila mzaliwa wa kwanza ambaye Waisraeli watanitolea, akiwa mzaliwa wa kwanza wa binadamu, au wa mnyama, atakuwa wako. Walakini huna budi kuwakomboa wazaliwa wa kwanza wote wa binadamu, na kila mzaliwa wa kwanza wa mnyama aliye najisi ni lazima akombolewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa mnyama, ambaye ametolewa kwa Mwenyezi Mungu ni wenu. Lakini ni lazima mtamkomboa kila mwana mzaliwa wa kwanza na kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wanyama wasio safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea Bwana cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kila mzaliwa wa kwanza ambaye Waisraeli watanitolea, akiwa mzaliwa wa kwanza wa binadamu, au wa mnyama, atakuwa wako. Walakini huna budi kuwakomboa wazaliwa wa kwanza wote wa binadamu, na kila mzaliwa wa kwanza wa mnyama aliye najisi ni lazima akombolewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa mnyama, ambaye ametolewa kwa BWANA ni wenu. Lakini ni lazima mumkomboe kila mwana mzaliwa wa kwanza na kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wanyama wasio safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa mnyama, ambaye ametolewa kwa bwana ni wenu. Lakini ni lazima mtamkomboa kila mwana mzaliwa wa kwanza na kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wanyama wasio safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsogezea BWANA cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kila mzaliwa wa kwanza ambaye Waisraeli watanitolea, akiwa mzaliwa wa kwanza wa binadamu, au wa mnyama, atakuwa wako. Walakini huna budi kuwakomboa wazaliwa wa kwanza wote wa binadamu, na kila mzaliwa wa kwanza wa mnyama aliye najisi ni lazima akombolewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye kila mwana wa kwanza wa mama yake, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga, atakuwa wako kwao wote walio wenye miili ya nyama, watu watakaomtolea Bwana, lakini mwana wa mtu utamtoa, akombolewe, vilevile mwana wa nyama aliye mwenye uchafu utamtoa, akombolewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea BWANA cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila muzaliwa wa kwanza ambaye Waisraeli watanitolea, akiwa muzaliwa wa kwanza wa wanadamu, au wa nyama, atakuwa wako. Lakini unaweza kuwakomboa wazaliwa wa kwanza wote wa wanadamu, na kila muzaliwa wa kwanza wa nyama anayekuwa muchafu.