Numbers 18:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Walawi peke yao ndio watakaohudumu katika hema la mkutano; na kuwajibika kikamilifu juu yake. Hili ni sharti la kudumu katika vizazi vyenu vyote. Walawi hawatakuwa na mali ya kurithi nchini Israeli,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni Walawi watakaofanya kazi katika Hema la Kukutania na kubeba wajibu wa makosa dhidi yake. Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. Hawatapokea urithi wowote miongoni mwa Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Walawi peke yao ndio watakaohudumu katika hema la mkutano; na kuwajibika kikamilifu juu yake. Hili ni sharti la kudumu katika vizazi vyenu vyote. Walawi hawatakuwa na mali ya kurithi nchini Israeli,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni Walawi watakaofanya kazi katika Hema la Kukutania na kubeba wajibu wa makosa dhidi yake. Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. Hawatapokea urithi wo wote miongoni mwa Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni Walawi watakaofanya kazi katika Hema la Kukutania na kubeba wajibu wa makosa dhidi yake. Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. Hawatapokea urithi wowote miongoni mwa Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Walawi peke yao ndio watakaohudumu katika hema la mkutano; na kuwajibika kikamilifu juu yake. Hili ni sharti la kudumu katika vizazi vyenu vyote. Walawi hawatakuwa na mali ya kurithi nchini Israeli,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila Walawi tu na wazifanye kazi za utumishi wa Hema la Mkutano, nao ndio watakaotwikwa manza, watakazozikora. Haya sharti yawe maongozi ya kale na kale ya kuviongoza vizazi vyenu, nanyi hamtapata fungu la nchi kuwa lenu katikati ya wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Walawi peke yao ndio watakaotumika katika hema la mukutano; na kuwa na mapaswa kwa ukamilifu juu yake. Hili ni sharti la kufuata siku zote katika vizazi vyenu vyote. Walawi hawatakuwa na mali ya kurizi katika inchi ya Israeli,