Numbers 18:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ninayowapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kuwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu, iwe zaka ya hiyo zaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ambayo ninawapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kama sadaka kwa BWANA, iwe zaka ya hiyo zaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ambayo ninawapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kama sadaka kwa bwana, iwe zaka ya hiyo zaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sema nao Walawi, uwaambie: Mtakapoyachukua mafungu ya kumi kwao wana wa Isiraeli, niliyowapa ninyi kuwa fungu lenu kwao, nanyi sharti mtoe humo vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana, navyo sharti viwe fungu la kumi la hayo mafungu ya kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena utawaambia Walawi maagizo haya: Wakati mutakapopokea sehemu ya kumi ambayo Yawe amewapa kutoka kwa Waisraeli ikuwe urizi wenu, mutanitolea mimi Yawe sehemu moja ya kumi ya vitu hivyo.