Numbers 18:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ndivyo mtakavyonitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za zaka mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Zaka hiyo mtakayonitolea mimi Mwenyezi-Mungu mtampa kuhani Aroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa njia hii, ninyi pia mtatoa sadaka kwa Mwenyezi Mungu kutoka zaka zote mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Kutoka kwa zaka hizi, ni lazima mtoe sehemu ya Mwenyezi Mungu kwa Haruni, kuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ndivyo mtakavyonitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za zaka mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Zaka hiyo mtakayonitolea mimi Mwenyezi-Mungu mtampa kuhani Aroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa njia hii ninyi pia mtatoa sadaka kwa BWANA kutoka katika zaka zote mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Kutoka kwenye zaka hizi, ni lazima mtoe sehemu ya BWANA kwa Aroni, kuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa njia hii, ninyi pia mtatoa sadaka kwa bwana kutoka zaka zote mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Kutoka kwenye zaka hizi, ni lazima mtoe sehemu ya bwana kwa Haruni, kuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ndivyo mtakavyonitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za zaka mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Zaka hiyo mtakayonitolea mimi Mwenyezi-Mungu mtampa kuhani Aroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mtakapovitoa hivyo vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana vya mafungu yenu ya kumi, mtakayoyachukua kwa wana wa Isiraeli, sharti m mpe mtambikaji Haroni hivyo vipaji vya tambiko, mtakavyovitoa kwenu vya kumnyanyulia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ndivyo, mutakavyonitolea mimi Yawe sadaka ya sehemu ya kumi mutakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Sehemu hiyo ya kumi mutakayonitolea mimi Yawe mutamupa kuhani Haruni.