Numbers 18:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo utawaambia: Mkishanitolea sehemu bora kuliko zote, sehemu itakayobakia itakuwa yenu, kama ilivyo kwa mkulima ambaye huchukua kinachobakia baada ya kutoa sadaka zake za mazao ya kwanza ya nafaka na zabibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waambie Walawi: ‘Mtakapotoa sehemu zilizo bora sana, itahesabiwa kwenu kama mazao ya sakafu ya kupuria nafaka, au ya shinikizo la kukamulia zabibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo utawaambia, Mtakapoinua humo hayo yaliyo mema, ndipo yatahesabiwa kuwa ya Walawi, kama kuongea kwake sakafu ya kupuria nafaka, na kama maongeo ya kinu cha kushindikia zabibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo utawaambia: Mkishanitolea sehemu bora kuliko zote, sehemu itakayobakia itakuwa yenu, kama ilivyo kwa mkulima ambaye huchukua kinachobakia baada ya kutoa sadaka zake za mazao ya kwanza ya nafaka na zabibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Waambie Walawi: ‘Wakati mtakapotoa sehemu zilizo bora sana, itahesabiwa kwenu kama mazao ya sakafu ya kupuria nafaka, au ya shinikizo la kukamulia zabibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waambie Walawi: ‘Mtakapotoa sehemu zilizo bora sana, itahesabiwa kwenu kama mazao ya sakafu ya kupuria nafaka, au ya shinikizo la kukamulia zabibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hayo utawaambia, Mtakapoinua humo hayo yaliyo mema, ndipo yatahesabiwa kuwa ya Walawi, kama mavuno ya sakafu ya kupuria nafaka, na kama mavuno ya kinu cha kusindikia zabibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo utawaambia: Mkishanitolea sehemu bora kuliko zote, sehemu itakayobakia itakuwa yenu, kama ilivyo kwa mkulima ambaye huchukua kinachobakia baada ya kutoa sadaka zake za mazao ya kwanza ya nafaka na zabibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo uwaambie: Mtakapotoa humo vilivyo vizuri zaidi kuwa vipaji vyenu vya tambiko vya kunyanyuliwa, vitawaziwa kuwa mapato ya Walawi ya mapurio yao na mapato ya makamulio yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo utawaambia, Mtakapoinua humo hayo yaliyo mema, ndipo yatahesabiwa kuwa ya Walawi, kama kuongea kwake sakafu ya kupuria nafaka, na kama maongeo ya kinu cha kushindikia zabibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo utawaambia: Mukisha kunitolea sehemu bora kuliko zote, sehemu itakayobakia itakuwa yenu, kama vile inavyokuwa kwa mulimaji anatwaa kinachobakia kisha kutoa sadaka zake za mazao ya kwanza ya ngano na zabibu.