Numbers 18:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni mimi niliyewachagua ndugu zenu Walawi miongoni mwa Waisraeli kama toleo kwenu. Wao wametengwa kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu, ili watoe huduma katika hema la mkutano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi mwenyewe nimewachagua Walawi wenzenu kutoka miongoni mwa Waisraeli kama zawadi kwenu, waliowekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu ili kufanya kazi katika Hema la Kukutania.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami, tazama, nimewatwaa ndugu zenu Walawi miongoni mwa wana wa Israeli; kwenu ninyi watu hao ni kipawa alichopewa Bwana, waufanye utumishi wa hema ya kukutania.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni mimi niliyewachagua ndugu zenu Walawi miongoni mwa Waisraeli kama toleo kwenu. Wao wametengwa kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu, ili watoe huduma katika hema la mkutano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi mwenyewe nimewachagua Walawi wenzenu kutoka miongoni mwa Waisraeli kama zawadi kwenu, waliowekwa wakfu kwa BWANA ili kufanya kazi katika Hema la Kukutania.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi mwenyewe nimewachagua Walawi wenzenu kutoka miongoni mwa Waisraeli kama zawadi kwenu, waliowekwa wakfu kwa bwana ili kufanya kazi katika Hema la Kukutania.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami, tazama, nimewatwaa ndugu zenu Walawi miongoni mwa wana wa Israeli; kwenu ninyi watu hao ni kipawa alichopewa BWANA, wahudumu katika hema ya kukutania.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni mimi niliyewachagua ndugu zenu Walawi miongoni mwa Waisraeli kama toleo kwenu. Wao wametengwa kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu, ili watoe huduma katika hema la mkutano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, mimi nimewatoa ndugu zenu Walawi katikati yao wana wa Isiraeli, nikawapa ninyi kuwa vipaji vya Bwana kwa kuutumikia utumishi wote wa Hema la Mkutano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami, tazama, nimewatwaa ndugu zenu Walawi miongoni mwa wana wa Israeli; kwenu ninyi watu hao ni kipawa alichopewa BWANA, waufanye utumishi wa hema ya kukutania.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mimi niliyewachagua wandugu zenu Walawi kati ya Waisraeli kama vile toleo kwenu. Wao wametengwa kwa ajili yangu mimi Yawe, kusudi wafanye kazi katika hema la mukutano.