Numbers 19:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Agusaye maiti, yaani mwili wa mtu aliyekufa, asipojitakasa, analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu, naye atatengwa na wana wa Israeli. Mtu huyo atabaki najisi kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya Mwenyezi Mungu. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Agusaye maiti, yaani mwili wa mtu aliyekufa, asipojitakasa, analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu, naye atatengwa na wana wa Israeli. Mtu huyo atabaki najisi kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu ye yote agusaye maiti ya mtu ye yote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya BWANA. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake hubaki juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya bwana. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu yeyote yule agusaye maiti ya mtu aliyekufa, asijitakase, analitia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ungali upo juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Agusaye maiti, yaani mwili wa mtu aliyekufa, asipojitakasa, analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu, naye atatengwa na wana wa Israeli. Mtu huyo atabaki najisi kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mtu atakayegusa mfu, ni kwamba maiti ya mtu ye yote aliyekufa, asipojieua hulichafua Kao la Bwana; mtu aliye hivyo sharti ang'olewe kwao Waisiraeli. Kwa kuwa hakunyunyiziwa hayo maji ya kunyunyiza, ni mwenye uchafu, nao huo uchafu wake utamkalia vivyo hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anayegusa maiti, ni kusema mwili wa mutu aliyekufa, asipojitakasa, anachafua hema la Yawe, naye atatengwa na watu wa Israeli. Mutu huyo atabaki muchafu kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.