Numbers 19:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Haya ni masharti ya sheria ambayo mimi Mwenyezi-Mungu ninatoa. Waambieni Waisraeli wawaletee ng'ombe jike mwekundu asiye na dosari wala kasoro yoyote, na ambaye hajapata kufungwa nira.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hivi ndivyo sheria ambayo Mwenyezi Mungu ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hii ndiyo amri ya sheria Bwana aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng'ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Haya ni masharti ya sheria ambayo mimi Mwenyezi-Mungu ninatoa. Waambieni Waisraeli wawaletee ng'ombe jike mwekundu asiye na dosari wala kasoro yoyote, na ambaye hajapata kufungwa nira.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hivi ndivyo sheria ambayo BWANA ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa na ambaye hajapata kufungwa nira.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hivi ndivyo sheria ambayo bwana ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng'ombe jike mwekundu asiye na doa, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Haya ni masharti ya sheria ambayo mimi Mwenyezi-Mungu ninatoa. Waambieni Waisraeli wawaletee ng'ombe jike mwekundu asiye na dosari wala kasoro yoyote, na ambaye hajapata kufungwa nira.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo maongozi ya mafunzo, Bwana aliyoyaagiza kwamba: Waambie wana wa Isiraeli, wakupatie ng'ombe mwekundu jike asiye na kilema wala doadoa lo lote, asiyefungwa bado kuvuta gari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ni masharti ya sheria ambayo mimi Yawe ninatoa. Uwaambie Waisraeli wawaletee ngombe dike mwekundu mukamilifu asiyekuwa na kilema chochote, na ambaye hajapata kufungwa nira.