Numbers 19:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu watalishika sharti hili daima. Mtu atakayenyunyiza maji ya kutakasia ataosha nguo zake; naye anayegusa maji hayo ya najisi atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ni agizo la kudumu kwao. “Mtu anayenyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote anayegusa maji ya utakaso atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo itakuwa amri ya sikuzote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hata jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu watalishika sharti hili daima. Mtu atakayenyunyiza maji ya kutakasia ataosha nguo zake; naye anayegusa maji hayo ya najisi atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ni sheria ya kudumu kwao. “Mtu ye yote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na ye yote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ni sheria ya kudumu kwao. “Mtu yeyote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo itakuwa amri ya siku zote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu watalishika sharti hili daima. Mtu atakayenyunyiza maji ya kutakasia ataosha nguo zake; naye anayegusa maji hayo ya najisi atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya yawe kwao maongozi ya kale na kale. Naye yule aliyemnyunyizia mwenzake hayo maji ya kunyunyiza sharti azifue nguo zake. Naye atakayeyagusa hayo maji ya kunyunyiza atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo itakuwa amri ya sikuzote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hata jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hili ni sharti la kufuata siku zote. Mutu atakayenyunyiza maji ya utakaso atafua nguo zake; naye atakayegusa maji hayo atakuwa muchafu mpaka magaribi.