Numbers 19:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chochote atakachogusa mtu najisi kitakuwa najisi, na yeyote atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi mpaka jioni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi hadi jioni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kitu cho chote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hata jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chochote atakachogusa mtu najisi kitakuwa najisi, na yeyote atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi mpaka jioni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kitu cho chote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na ye yote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kitu chochote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chochote atakachogusa mtu najisi kitakuwa najisi, na yeyote atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi mpaka jioni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyote, mwenye uchafu atakavyovigusa, vitakuwa vyenye uchafu, naye kila mtu, atakayemgusa, atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kitu cho chote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hata jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chochote mutu muchafu atakachogusa kitakuwa kichafu, na yeyote atakayekigusa kitu hicho atakuwa muchafu mpaka magaribi.