Numbers 19:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu aliye safi atayazoa majivu ya ng'ombe huyo na kuyapeleka mahali safi nje ya kambi. Yatahifadhiwa na kutumiwa na jumuiya nzima ya Israeli kutengeneza maji ya kuondoa najisi, ili kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtu ambaye ametakaswa atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali nje ya kambi palipo safi. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Waisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng'ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu aliye safi atayazoa majivu ya ng'ombe huyo na kuyapeleka mahali safi nje ya kambi. Yatahifadhiwa na kutumiwa na jumuiya nzima ya Israeli kutengeneza maji ya kuondoa najisi, ili kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng'ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa Israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu aliye safi atayazoa majivu ya ng'ombe huyo na kuyapeleka mahali safi nje ya kambi. Yatahifadhiwa na kutumiwa na jumuiya nzima ya Israeli kutengeneza maji ya kuondoa najisi, ili kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mtu mwenye kutakata na ayazoe majivu yake huyo ng'ombe, ayaweke nje ya makambi mahali palipo penye kutakata, yakae hapo hapo na kuangaliwa, yawe tayari, mkutano wa wana wa Isiraeli watakapoyatumia ya kutengeneza maji ya kunyunyiza, kwani ni ng'ombe ya tambiko ya weuo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng’ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu anayekuwa safi atazoa majivu ya ngombe huyo na kuyapeleka pahali safi inje ya kambi. Yatalindwa na kutumiwa na jamii nzima ya Israeli kwa kutengeneza maji ya utakaso kwa kuondoa zambi.